Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, April 5 2016 jina lake limerudi kwenye headlines kwa mara nyingine tena. Rais Magufuli amerudi kwenye headlines baada ya kukubali mwaliko wa Rais Paul Kagame wa Rwanda, hivyo atafanya ziara ya siku mbili Jumatano na Alhamisi.
Stori kutoka wizara ya mambo ya nje zinaeleza kuwa Rais Magufuli pamoja na Rais Kagame watafungua daraja la kimataifa la Rusumo linaounganisha mpaka wa Tanzania na Rwanda na kuzindua ushirikiano wa huduma za kituo cha pamoja.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na kusomwa katika television za Tanzania Rais Magufuli atasafiri kwa gari.
Rais Magufuli pia atakwenda kuweka shada katika makaburi ya mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 na baadae kufanya mazungumzo ya pamoja na Rais Kagame mjini Kigali. Hii ndio itakuwa safari ya kwanza ya Rais Magufuli kusafiri nje ya nchi toka aingie madarakani October 2015.
ULIIKOSA HII? MATANO YA KUFAHAMU KUHUSU DARAJA LA KIGAMBONI KABLA HALIJAANZA KUTUMIKA MWEZI HUU? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE