Msanii maarufu wa hiphop kutoka Marekani T.I anaziandika headlines siku ya leo, baada ya kukaa chini ya carptet kwenye headlines za vyombo vya Sheria kwa muda, kwa bahati mbaya urafiki wake na vyombo vya kulipa kodi ‘IRS’ vya Marekani upo matatani.
IRIS inamshitaki msanii huyo wa Hiphop maarufu kama The King of Atlanta kwa deni la dola Million 4.5 (zaidi ya Tzs. Billion 900 ) ya kodi, na hii itakuwa mara ya tatu kwa T.I kudaiwa kodi na IRS, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2012 alidaiwa dola Millioni 1,397,283 na mwaka 2013 alidaiwa dola Million 3,173,476.
Mwaka 2014 T.I alikuwa salama kabisa IRS haikuwa na cha kumdai lakini mwaka huu mambo hayajaenda vizuri, IRS imekuja juu na kudai kuwa msanii huyo alilipa kiasi cha fedha za kodi lakini kwa miezi kadha amekuwa akilipoteza deni lililobaki la dola Million 4.3 na wanashangazwa anavyofungua biashara mpya kila kukicha lakini kulipa hiyo Millioni 4.3 inakuwa tatizo.
Kwasababu hiyo T.I yupo matatani kufilisiwa baadhi ya mali zake kwani IRS imesema kama akiendelea kukwepa kulipa deni hilo basi watalazimika kusimamisha baadhi ya biashara zake ama kuuza baadhi ya mali zake ili kurudisha hela wanaomdai msanii huyo.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos