Kuna mpango wa kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Anga Tanzania kwenye eneo la kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro (KIA), wenye utaalamu wao wanasema mpango huo utasaidia kiasi kikubwa kuimarisha Shirika la Ndege la Tanzania kwa kuwa na Marubani wake wenyewe ambao watapata mafunzo hapahapa nchini kwa gharama nafuu tofauti na ilivyo sasa.
Kwa mudu mrefu tangu Tanzania ipate uhuru, hakujawa na Chuo Kikuu cha Urubani kitu ambacho kimewalazimu wale wote wenye wanaotaka kujifunza Urubani wasafiri mpaka nje ya Nchi, sasa baada ya jitihada za Serikali ya awamu ya tano kufufua Shirika la Ndege imeonekana ni muhimu jitihada hizo zikaenda sambamba na Uanzishwaji wa hiki Chuo kikuu.
Chuo hicho ambacho kitakuwa sehemu ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimependekezwa kujengwa katika eneo la uwanja wa KIA kwenye Mkoa wa Kilimanjaro kutokana na miundombinu muhimu ya mafunzo kwa vitendo pamoja na eneo la kutosha ambapo tayari tunavyoongea, zaidi ya hekta 60 zimeshatengwa na Uongozi wa KIA kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na miundombinu mingine muhimu kwa ajili ya Chuo hicho.
Tayari baadhi ya Wabia muhimu katika mpango huu likiwemo Taifa la China na Afrika ya Kusini wamefika katika eneo la KIA kwa ajili ya ukaguzi wa awali kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Chuo hicho ambacho kitakua Chuo Kikuu cha kwanza cha mafunzo ya urubani nchini Tanzania.
HD VIDEO: RC ALLY HAPI ALIVYOFOKA, TAZAMA ALIVYOAGIZA MENEJA WA BENKI NA MWANASHERIA WA BENKI WACHUKULIWE NA POLISI, BONYEZA PLAY KUONA MKASA MZIMA KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI