Ni Mkuu wa Mkoa wa DSM, Aboubakar Kunenge ambae leo Octoba 28, 2020 amejiunga na wananchi katika zoezi la upigaji kura
‘Nimefika kuja kukamilisha haki yetu ya kikatiba, Wananchi wamejitokeza kwa wingi kwaajili ya kupiga kura na zoezi linaendelea vizuri, kiukweli tangu nitoke nyumbani mpaka hapa sijakutana na hali yoyote ya Vurugu hali ni shwari kabisa na wala hakuna tukio lililovunja Amani’-RC Kunenge
‘Hali ni shwari na ninaomba wananchi wengine ambao wapo majumbani waje kupiga kura kwani ni haki ya kila mwananchi’- RC Kunenge