Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amoss Makala amesema haitokuwa sawa Watu wasifanye kazi kisa kuna usafi na kusema licha ya kuzinduliwa kwa kampeni ya usafi maduka hayapaswi kufungwa kisa kufanya usafi.
Kupitia Clouds360 ya CloudsTV leo Makalla amesema ———”Jana tulizindua kitabu cha mwongozo niwashukuru sana Wadau wote ambao wameunga mkono kampeni hii ya usafi katika Mkoa wa Dar es Salaam, huu mwongozo wangu unataka tufanye usafi kuanzia saa 12 na nusu mpaka saa tatu, ule mwanzo ulikuwa unakwenda hadi saa nne asubuhi tena na maduka yasifunguliwe”
“Tuchukulie mfano Mtu anakwenda machinjioni aamke saa 10 akachinje ng’ombe halafu tukitoka kwenye usafi ndio tunywe supu huyu naye tuseme aende machinjioni saa tatu atakuta ng’ombe?, ni busara tu ya kawaida, lakini anayekwenda machinjioni kule kwenye kaya si ana Ndugu si wanafanya usafi?.
WAVAMIZI WAUA TWIGA, SWALA “WACHOMA SHAMBA, MALI ZAIDI MILIONI 60 ZATEKETEA”