Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ameagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Zefrin Lubuva asilipwe mshahara wa Februari hadi atakapojirekebisha.
Mkurugenzi huyo alishindwa kujibu kwanini Halmashauri hiyo imeshindwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya Wanawake, Vijana na Walemavu.
Sakata hilo limetokea February 14, katika kikao maalumu cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa cha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021.
Mama Mghwira “Mkurugenzi wa Mwanga kila wakati umekuwa ukishindwa kujibu maswali vile inavyopaswa, sijajua ni nani anakulipa mshahara, ila mamlaka inayohusika kukulipa isikulipe mshahara wa mwezi huu,”.
Kila Halmashauri hutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuwapa mikopo isiyo na riba Vijana, Walemavu na Wanawake.