Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amewaonya wamachinga ambao wamekua wakifanya biashara katika maeneo yasiyostahili kuhakikisha wanaenda katika eneo la soko la Mwanjelwa ambalo wametengewa.
“Kuna wenzetu Wamachinga wa kaeneo Kamwanjelwa, Kabwe na City garden msimamo wangu kama RC huko vilevile haujawahi kubadilika kwamba eneo hilo ni eneo ambalo hawapaswi hata kidogo na ninazungumza kwenu with confidence nimesikia mahali fulani kuna baadhi ya watu wanasema warudi, anayesikilizwa katika masuala haya ni Serikali’ RC Chalamila
“Wasitafute vilio na ninasema ukweli na kama kuna Kiongozi ana muwasho wa aina yoyote ni vizuri kutumia muda wa kuyawasilisha hayo mahali panapo stahili” RC Chalamila
BREAKING: KAMANDA TABORA ANAZUNGUMZIA WATU WATANO NDUGU WALIUAWA KWA RADI