Mix

Ridhiwani Kikwete ajibu kuhusu kuchunguzwa kwake sakata la dawa za kulevya

on

Sakata la dawa za kulevya bado limeendelea kushika kasi Tanzania Serikali ikiendelea kuwachunguza baadhi ya Watuhumiwa wa matumizi na Wafanyabiashara.

Moja ya habari kubwa kupitia Magazeti na vyombo vya habari leo ni taarifa za kuhusishwa kwa Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete, tuhuma hizo zimemfikia hata yeye mwenyewe na akaamua kuchukua time yake kuzijibu kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ridhiwan ameandika>>>’Ni jambo jema na la faraja kubwa kwangu kama uchunguzi unafanywa, ni ukombozi kwangu, ukweli utajulikana kuwa ni uvumi tu usiokuwa na chembe ya ukweli”

“Ni maneno ya watu wasionitakia mema, sina la kuficha… sifanyi biashara hiyo haramu na wala sijawahi kufikiria kufanya…… ni bora kufa maskini kuliko kutafuta utajiri kwa njia hiyo.’

VIDEO: “Unapotangaza mtu aje Polisi saa 5, wewe ni nani? – FREEMAN MBOWE… bonyeza play kwenye hii video hapa chini kumtazama Mbowe akizungumza yote baada ya kutajwa na Mkuu wa mkoa Paul Makonda

Soma na hizi

Tupia Comments