MAHAKAMA Kuu Kanda ya DSM leo July 6, 2017 imeahirisha kusikiliza kesi ya Bodi Mpya ya Wadhamini wa Chama cha Wananchi, CUF iliyosajiliwa hivi karibuni na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini RITA ambayo ilipendekezwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.
Bodi hiyo iliwasilisha Mahakamani hapo maombi ya kufuta kesi zote za chama hicho zilizofunguliwa na Bodi iliyomaliza muda wake ambayo ilikuwa upande wa Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad zinazohusiana na mgogoro wa uongozi ndani ya chama.
Jaji Dyansobera aliahirisha shauri hilo hadi Jumatatu July 10, 2017.
“Tulikuwa Mahakamani mbele ya Jaji kwa ajili ya kusikiliza leo shauri la Chama cha Wananchi CUF kuhusiana na suala la ruzuku. Tulivyokuwa Mahakamani tarehe ya mwisho iliamriwa tuje leo kwa ajili ya kusikiliza pingamizi. Amri iliyotoka siku ile ilikuwa lile pingamizi walilokuwa wameliweka upande wa Serikali tupatiwe nakala sisi upande wa Chama cha Wananchi CUF.” – Wakili Juma Nassoro.
Tamko la TCRA kwa makampuni ya simu Tanzania!!!