Club ya Real Madrid ya Hispania leo imetangaza rasmi kuwepo na makato ya mishahara ya wachezaji wake kwa asilimia 10 hadi 20 wakati huu wa janga la virusi vya corona.
Uamuzi huo wa Real Madrid utawahusu sio tu wachezaji bali hadi benchi la ufundi, hiyo pia itategemeana na msimu huo wa Ligi 2019/20 utamalizika lini.
Real Madrid sio club ya kwanza Ulaya kutangaza kuamua kuwakata mishahara wachezaji wake, FC Barcelona imewakata wachezaji wake mishahara kwa asilimia 70 ili iweze kuwalipa staff wengine wakati huu wa janga la corona.