Msimu mpya wa ligi ya mabingwa wa ulaya umefunguliwa leo rasmi kwa michezo 8 kuchezwa katika viwanja tofauti barani humo.
Mabingwa wa kihistoria wa kombe hilo, klabu ya Real Madrid ikiwa nyumbani katika dimba la Santiago Bernabeu leo imefungua michuano hiyo kwa ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Shakhtar Donestski ya Ukraine.
Akitoka kufunga magoli matano katika mchezo uliopita wa jumamosi, mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo leo alifunga magoli matatu kati manne ya Madrid, huku Karim Benzema akifunga lingine.
Benzema alianza kufunga dakika ya 30, Ronaldo akaongeza mengine dakika ya 55’ (p), 63’ (p), 81’ na hivyo kuweka rekodi ya kufunga jumla ya magoli 80 katika historia ya michuano hiyo.
Magoli matati ya leo yanamfanya Ronaldo kuwa mfungaji bora wa muda wa Champions League huku akifikisha jumla ya magoli 500 tangu aanze kucheza soka la ushindani.