Toka nimeanza kufatilia hii chati ya TRACE TV, kituo cha ufaransa ambacho kimeshika hata nchi za Afrika kwa kucheza muziki wenye viwango kutoka kila kona ya dunia, sijawahi kuona msanii wa Afrika Mashariki alieshika nafasi ya kwanza kwenye Top10.
Siku zote nilizoea kuona Wasouth Africa na Wanigeria ndio wanaishika namba 1 ila sasa Mtanzania Diamond ameivunja hiyo rekodi kupitia single yake ya ‘number 1 rmx’ ambayo kamshirikisha Mnigeria Davido
Namba 2 ni Davido – Aye
Namba 3 ni Burna Boy – Yawa Dey
Namba 4 ni Khuli Chana – Wannabeez
Namba 5 ni R2bees “Love”
Namba 6 ni Oshee ya Praiz ft Awilo
Namba 7 ni 2 face na T Pain
Namba 8 ni Jimmy Nevis Ft. Kwesta Balloon
Namba 9 ni hii hapa chini ya Skelewu ya Davido
Hii hapa chini ndio namba 10 – Rands and nairas – Emmy Gee ft AB Crazy & Dj Dimplez
Kama unataka usipitwe na stori kama hizi, karibu ujiunge na familia ya millardayo.com kupitia facebook, twitter na instagram kwa jina hilohilo la @millardayo