April 12, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa reli ya kisasa standard gauge kutoka jijini Dar es Salaam hadi Morogoro.
'Ujenzi wa reli huwa ni gharama kubwa, reli hii itakuwa inabeba uzito mkubwa na spidi kubwa, watu watalala Moro na watafanya kazi DSM'-JPM
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Ujenzi wa reli ya kisasa utakuza sekta zingine nchini, itawezesha malighafi mbalimbali kusafirishwa kwenda kwenye maeneo ya viwanda'-JPM
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Ujenzi wa reli hii ya kisasa utasaidia kutunza barabara zetu, barabara zetu zinaharibika kwa sababu zinasafirisha mizigo mikubwa'-JPM
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa unatarajiwa kutoa ajira kwa watu takribani 600,000'-Rais Magufuli #MillardAyoUPDATES
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 30'-Rais Magufuli #MillardAyoUPDATES #UjenziRELIYAKISASA
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Wale wataalamu wa kusoma kwenye mitandao wakaangalie ni nchi gani imejenga reli ya namna hii kwa pesa zake watakuta ni Tanzania'-JPM
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Unapokuwa dereva wa lori na unapopakia abiria hutakiwi kuwauliza wasimame waangalie sehemu gani, dereva mzuri anangalia kufika salama'-JPM
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Nawahakikishia Watanzania mimi ni dereva mzuri nawahakikishia lori litafika kule tunakokwenda na hili ni lori la maendeleo'-JPM
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Kazi tunazozifanya mara nyingi utakaowaona wanapiga kelele ni wale ambao walizoea kupiga dili, na mimi nataka waendelee kupiga kelele'-JPM
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Tanzania imekuwa kwa uchumi 7%, ushahidi wa kukua kwa uchumi ndio hii miundombinu tunayoijenga'- Rais Magufuli
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Hivi karibuni tumepata mkopo wa kuanza kujenga barabara za mwendokasi katika awamu ya tatu na ya nne'-Rais Magufuli #MillardAyoUPDATES
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Tunajua tunapoenda pasitokee mtu wa kubadilisha ajenda tuanze kuzungumzia ajenda ambazo hazipo kwenye ilani ya uchaguzi'-Rais Magufuli
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Nataka mhandisi amalize mradi wa reli ya kisasa kabla ya miezi 30, na ikiwezekana siku ya kufungua twende bure mpaka Dodoma'-Rais Magufuli
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Vita ya kupambana na ufisadi ni ngumu na hasa unapowabadilisha watu wachache waliozoea maisha fulani kwa miaka 50'-Rais Magufuli
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Wanasema samaki mkunje akiwa mbichi, fisadi mkunje akiwa mbichi akishakomaa mvunje, nafuu walalamike wachache, Watanzania wafurahi'-JPM
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Nazuia hata michanga ya madini, ninafanya kazi hii kwa niaba yenu, kwani nashindwa kusema nipelekee hiyo michanga nitaikuta Ulaya?'-JPM
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Mlinituma nifanye haya, au niwaulize ndugu zangu haya yote ninayoyafanya kweli ni mabaya?'- Rais Magufuli #MillardAyoUPDATES
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Niko kwa niaba yenu, tumeonewa sana, Tanzania ni tajiri hatutakiwi kuwa ombaomba'- Rais Magufuli #MillardAyoUPDATES
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Tanzania tunaweza kwa hiyo tunapoyafanya haya tunafanya kwa sababu tuna wajibu wa kufanya, na haya ni malipo yangu kwenu'-Rais Magufuli
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Watanzania wanataka maendeleo, hakuna anayekula siasa kwa hiyo Tanzania kwanza siasa baadae'-Rais Magufuli #MillardAyoUPDATES
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
'Niwaombe tuangalie TZ kwanza siasa baadae, muiache Serikali ya CCM iliyoaminiwa na Watanzania itekeleze wajibu wake tutakutana 2020'-JPM
— millardayo (@millardayo) April 12, 2017
VIDEO: Rais Magufuli amezindua ujenzi wa Reli ya kisasa DSM-Morogoro. Bonyeza play kutazama.