Wataalamu wa afya kila siku husisitiza kufanya mazoezi hata kwa muda wa nusu saa kwa ajili ya kujiepusha na magonjwa mbalimbali ambapo leo April 17, 2017 nimekutana na stori hii ambayo unaambiwa, kwa kila saa moja unayokimbia huongeza muda wa kuishi kwa saa saba, kwa mujibu wa utafiti mpya.
Kwenye taarifa iliyochapishwa na Daily Mail April 12, 2017 wanasayansi wanasema kukimbia kwa saa moja kwa wiki ni mazoezi tosha ya kuongeza muda wa kuishi bila kujali unakimbia kwa umbali gani au unakimbia kwa kasi gani ambapo watu wanaouchukua ushauri huu kwa moyo mmoja na kukimbia kila siku, huweza kuongeza muda wa kuishi wa hadi siku tatu.
Utafiti uliofanywa Iowa State University, ulirudia kuchambua data kutoka Cooper Institute, mjini Texas, na kufuatilia matokeo katika tafiti mbalimbali za karibuni ambazo zinahusiana baina ya mazoezi na muda wa kuishi ambapo walibaini kuwa kukimbia kwa angalau dakika saba kwa siku husaidia kuondoa uwezekano wa kufa kutokana na magonjwa ya moyo.
Baada ya kuchambua data za utafiti mpya, wanasayansi wanadai kuwa saa baada ya saa, kukimbia kwa takwimu hurejesha zaidi muda wa maisha ya watu kuliko kuuchukua.
AyoTV MAGAZETI: Kilichoandikwa kwenye magazeti ya April 17, 2017. Bonyeza play kutazama.