Kuna matukio ambayo yamezoeleka kufanywa na binadamu lakini inapokuja suala la wanyama kuwekewa sheria ambazo zimekuwa zikitumiwa na binadamu, jambo hilo huleta maswali mengi kama hii ya nchi ya Iran iliyoamua kuweka sheria kwa Ngamia kuwa na Plate Numbers ili kupunguza matukio ya ajali.
Mpaka sasa inaelezwa kuwa tayari wanyama takribani laki moja nchini Iran wamepewa namba za usajili huku wengine 35,000 wakipangwa kusajiliwa kabla ya mwaka huu kumalizika, na sababu kubwa ya kufanya hivyo imetajwa kuwa kuongezeka kwa matukio ya ajali za barabarani.
Maafisa wa usalama nchini Iran wameanza kutekeleza sheria hiyo kwa majaribio kwenye miji ya Sistan na Baluchestan ambayo iko mpakani mwa Afghanistan na Pakistan ambako kumekuwa na matukio ya uharibifu wa mali na ajali za mara kwa mara.
Mohammad-Sharif Khaleqinia, ambaye ni katibu mkuu wa Central Task Force ameuambia mtandao wa IRNA: “Tunatarajia kutoa namba za usajili kwa wanyama aina ya Ngamia wapatao 35,000 mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu, lengo letu ni kutaka kutambua mmiliki halali wa wanyama hawa”.
Kwa mujibu wa IFP News, lengo lingine la serikali ya Iran ni kuwafanya wananchi watimize majukumu yao ya kutunza wanyama wanaowafuga ikiwa ni pamoja na kupunguza au kuondoa kabisa wanyama wanaozurula mitaani na kusababisha usumbufu.
VIDEO: Uliikosa hii ya RC Paul Makonda wakati akisukuma magari mabovu aliyoyakuta ofisini kwake? Tazama hapa