Nani amesema umechelewa kuoa au kuolewa? kuna watu huwa na wasiwasi kuwa wamechelewa kufunga ndoa kwa madai umri umekwenda lakini kwa George Kirby na Doreen Luckie imekua tofauti kabisa baada ya kuamua kufunga ndoa wakiwa na umri mkubwa.
George mwenye miaka 103 na Doreen mwenye miaka 91 waliamua kutimiza ndoto yao hiyo ya siku nyingi kwa kufunga ndoa.
Wawili hao wamefunga ndoa baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa miaka 27 huku kila mmoja akisema hajutii kuchelewa kufanya maamuzi hayo.
Sherehe hiyo ya aina yake ambayo ilifanyika katika hotel ya Eastbourne, Kusini mwa Uingereza ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo ndugu na marafiki wa karibu wa familia hiyo.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.