Duniani

#RIP mtu mfupi zaidi Duniani, anaefatia kushika rekodi hiyo ??

on

Headlines zilibeba stori kubwa November 13 2014 kuhusu Sultan Kosen, raia wa Uturuki ambae ndio mtu mrefu zaidi Duniani pamoja na Chandra Dangi Raia wa Nepal ambaye alikuwa anashikilia Rekodi ya kuwa mtu mfupi zaidi Duniani walipokutana kwa mara ya kwanza Uingereza kwenye Maadhimisho ya Guinness World Record Day.

t5

Stori ya kusikitisha ni kwamba nafasi ya Rekodi ya mtu mfupi zaidi Duniani inabaki wazi kwa sasa baada ya Chandra Bahadur Dangi kufariki akiwa na umri wa miaka 75.

Baada ya Chandra kufariki sasa ni zaidi ya siku tano na bado hakuna jibu la nani atakayefikia rekodi aliyoweka ya kuwa mtu mfupi zaidi kuwahi kutokea Duniani ambapo alikuwa na Urefu wa inch 21.5.

Picha nyingine kumbukumbu ya kukutana kwa Chandra na Sultan hizi hapa mtu wangu.
t1

t2

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments