Kutoka Karimjee Dar alivyoagwa Marehemu Dk. Abdallah Kigoda, mazishi ni leo Tanga
Share
3 Min Read
SHARE
Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania, Dk. Abdallah Omar Kigodauliwasili jana October 14 2015, kutoka India ambako Waziri huyo alifariki wakati akipatiwa Matibabu.
Mwili ulihifadhiwa katika Hospitali ya Kijeshi ya Lugalo Dar e Salaam, leo October 15 2015 mwili wa Marehemu Dk. Kigoda umefikishwa katika Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam ambapo watu mbalimbali wakiongozwa na baadhi ya Viongozi wa Juu wa Serikali, ndugu na jamaa wametoa heshima za mwisho na kumuaga Marehemu Kigoda, safari ikaanza kuelekea Tanga kwa ajili ya Mazishi.
.Baadhi ya Viongozi waliohudhuria kuaga Mwili wa Dk. Kigoda, yuko Mzee Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal, Spika wa Bunge Mama Anne Makinda, Mzee Benjamin Mkapa, Balozi Ombeni Sefue, na Mama Anna Mkapa.Hawa nao ni waombolezaji wengine pia.Mwili wa Dk. Kigoda ukaingizwa ndani ya Ukumbi kwa ajili ya kuagwa.......Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho.Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho.Spika wa Bunge anayemaliza muda wake, Mama Anne Makinda.Rais Mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi.Rais Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa.Mama Anna Mkapaakitoa heshima za mwisho.Mwanadiplomasia Dr. Salim Ahmed Salim.Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Jaji Francis Mutungi akitoa heshima za mwisho pia.Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Said Meck Sadick......Mbunge wa Temeke, Abas Zuberi Mtemvu akisalimiana na mmoja wa waombolezaji.
Mwenyezi MUNGU ampumzishe kwa amani Dk. Abdallah Omar Kigoda.. #RIP
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTER FB YOUTUBE