Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said amefariki dunia mapema leo asubuhi akiwa katika mazoezi ya kuogelea.
Msemaji wa Mamlaka ya viwanja vya ndege Ramadhani Maleta amesema baada ya tukio hilo Bwa.Suleiman alikimbizwa hospitali ya Agakhan kwa matibabu na baadae ikaelezwa kuwa amekwishafariki na mazishi yake yanatarajiwa kufanyika leo jioni.
Marehemu pia aliwahi kuwa Katibu mkuu wa klabu ya Simba miaka ya zamani.
#MillardAyoUPDATES Mkurugenzi mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege TZ Mhandisi Suleiman Said amefariki dunia akiwa kwenye klabu ya kuogelea.
— millard ayo (@millardayo) January 18, 2016