Kikosi cha Real Madrid kimekuwa katika wiki ngumu baada ya kupoteza mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Atletico Madrid ambapo walifungwa mabao manne na wakajikuta wakiingia kwenye tatizo la kinidhamu baada ya wachezaji kadhaa akiwemo Cristiano Ronaldo kuonekana wakila bata saa chache baada ya kufungwa.
Katika hali ya kawaida nyakati kama hizi huwa ngumu kwa kocha na wachezaji au timu kwa jumla na ni nyakati ambazo wachezaji kadhaa hujitokeza kama viongozi na kuwaonyesha wenzao njia ya kupita ili kurudi kwenye mstari.
Kocha wa Real Madrid Mtaliano Carlo Ancelotti amewataja wachezaji watano kuwa ndio hasa wenye jukumu la kuwaongoza wenzao ndani ya kikosi hiki cha mabingwa wa Ulaya.
Ancelotti amemtaja mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo kuwa ni moja kati ya watu ambao ni viongozi kwenye timu yake ambapo amekuwa na jukumu la kuzungumza na kunyanyua ari ya wenzake hasa pale ambapo mambo hayaendi sawa.
Ancelotti amemtaja Ronaldo kuwa tegemeo linapokuja suala la kuwaongoza wenzie na amekuwa aina ya mtu ambaye kama yeye hayuko sawa mara nyingi timu yote pia hufuata kile kinachomtokea.
Kocha huyu mtaliano pia amewataja mabeki Peoe na Sergio Ramos kuwa viongozi kama ilivyo kwa Ronaldo kutokana na uzoefu wao na muda ambao wamecheza ndani ya timu hii pamoja na ukubwa wao ndani ya chumba cha kubadilisha nguo na heshima wanayopewa na wachezaji wenzao.
Viongozi wengine kwenye timu hii ni kipa Iker Cassilas na beki Mbrazil, Marcelo ambaye ni moja kati ya watu waliocheza muda mrefu ndani ya kikosi cha Real Madrid.
Katika mpangilio wa manidha wa Real Madrid kipa Iker Cassilas ndiye nahodha wa kwanza na msaidizi wake ni Sergio Ramos huku Marcelo akiwa nahodha wa tatu na Ronaldo ni nahodha wa nne.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook