Ukitaka kujua muziki mzuri unaokubalika mitaani kuna sehemu za kupita alafu unatoka na majibu kamili kabisa, moja ya sehemu hizo ni Club.. ukikatisha Club sio rahisi kukuta DJ kapiga midundo yote kwenye playlist alafu akaiacha ngoma ya AMARULA ambayo imeimbwa na mkali kutoka Zambia, Roberto.
Niliipata story kwamba jamaa anatua Mwanza, nikaona hata nisipitwe !! Kuna sababu zote kumshuhudia huyu mkali kutoka Zambia.. Kingine ni kwamba katika nchi ambazo zinafanya poa na tunasikiliza muziki wake, majina ya Wasanii toka Zambia hayasikiki kwa uzito mkubwa kama ilivyo kwa South Africa, Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria na nchi nyingine.
Nimeishuhudia show ya kwanza ya Roberto ndani ya TZ +255 ambayo imefanyika Jijini Mwanza, Jembe Beach… ilikuwa burudani kwa watu wa nguvu wa 88.1 Rock City Mwanza.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM,TWITTER,FB, YOUTUBE