Baada ya uwepo wa tambo za mashabiki wa soka wa pande za Real Madrid na FC Barcelona kwa zaidi ya wiki moja kuhusu mchezo wa marudiano wa EL Clasico, usiku wa April 2 ilikuwa ni zamu ya kupata majibu ya tambo za mashabiki wa pande zote.
Ukiachana na ushabiki, takwimu za karibuni za vilabu hivyo zilikuwa zinaonesha yoyote anaweza akashinda, kwani timu zote mbili mechi zao tano zilizopita kila timu wamepata ushindi, ila katika mechi tano walizocheza dhidi yao FC Barcelona alikuwa kashinda mara tatu na Madrid mara mbili.
Haikushangaza kuona Real Madrid inaondoka na point tatu kwa kushinda goli 2-1 katika uwanja wa Camp Nou, FC Barcelona ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 56 kupitia kwa Gerard Pique, ila dakika saba baadae Karim Benzema akasawazisha na Cristiano Ronaldo akafunga goli la ushindi kwa Madrid dakika ya 85.
Licha ya kuwa Real Madrid hawana matumaini ya kutwaa taji la Laliga msimu huu, Cristiano Ronaldo ameonesha furaha ya kupitiliza baada ya kusherekea ushindi katika vyumba vya kubadilishia nguo akiwa na nguo ya ndani pekee.
Video ya magoli ya FC Barcelona Vs Real Madrid, Full Time 1-2
https://youtu.be/00HoDckbeS0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE