Michezo

Cristiano Ronaldo kwenye movie? jibu ni YES !! Trailer yake imenifikia hapa…

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo mwezi June mwaka 2015 aliingia katika headlines baada ya kukiri kuwa amecheza movie inayohusu maisha yake na itatoka kabla ya mwaka 2015 haujamalizika. June 9 2015 mtandao wa bleacherreport.com uliandika kuhusiana na stori hii.

Ronaldo-Poster

September 28  Cristiano Ronaldo amerudi katika headlines baada ya kuachia trailer ya movie yake, movie ambayo ilichukua zaidi ya miezi 14 kuitengeneza, movie hiyo imepewa jina rahisi na staa huyo wa soka, kwani inaitwa jina halisi la staa huyo “Ronaldo” . Movie ya Cristiano Ronaldo ni movie ambayo kwa asilimia kubwa inahusu maisha yake halisi.

Ronaldo-Film-Trailer (1)Baadhi ya vipande vinavyoonekana katika trailer ya movie hiyo, staa huyo anaonekana akiwa na mtoto wake wa kiume Cristiano Ronaldo Junior na kusema kuwa anatamani kuwa golikipa, kitu ambacho Ronaldo anaonekana kushangazwa na nafasi anayotaka kucheza mtoto wake.

Ronaldo-Film-Trailer (4)

Ronaldo-Film-Trailer (2)Hii ni Trailer ya movie hiyo mtu wangu

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTERFBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments