Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana September 14, 2017 ilimuachia huru Mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya Manji na wenzake.
Akizungumzia suala hilo kisheria Wakili wa Kujitegemea Jebra Kambole ameeleza kuwa Sheria inampa mamlaka Mkurugenzi wa Mashtaka anaweza kumshtaki mtu yeyote lakini pia kuondoa shauri lolote mahakamani kwa wakati wowote.
“Hata hivyo kufuta shtaka hilo haimaanishi kwamba hawezi kukamatwa tena, DPP anaweza tena kuamuru mtu huyo akamatwe na afunguliwe mashtaka upya ila anatakiwa tu kuzingatia kutenda haki, maslahi ya umma, na kutokiuka utaratibu kulingana katiba ya nchi.” – Jebra Kambole
Ulipitwa na hii? BREAKING: Mahakama ya Kisutu imemuachia huru Yusuf Manji
Hii je?Kilichoikasirisha Mahakama kwenye kesi ya Sethi Sept 14