Siku ya August 6, 2017 Rais JPM alitoa kauli ya kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji dhidi ya watu waliouziwa viwanda na kuvitelekeza ambapo alimtaka Waziri Mwijage kuwanyang’anya na kuwapatia wawekezaji watao viendeleza.
Sasa leo August 7, 2017 Waziri wa Viwanda Charles Mwijage amehojiwa kwenye Clouds 360 Clouds TV na kuelezea kuhusu hiyo kauli ya rais na kutoa hizi kauli.
…>>>”Kujenga viwanda sio mchezo, yapo maelekezo ya Rais viwanda vilivyo binafsishwa na havitumiki virudishwe, Rais alichokitegemea kwangu sio kile anachokiona sababu viwanda haviendi kwa kasi anayoiona na hii kuna sababu kadhaa.”
“Hii sekta ya viwanda ni multi-sector maana kuna viwanda vipo chini ya Wizara ya Mifugo, vingine maliasili…. kuna viwanda vimechukuliwa lakini havipo kwenye list ya viwanda vilivyobinafsishwa, nahitaji Wakuu wa mikoa waingie hapa.”
“Kuna watu wengine wameingia kwenye sekta ya viwanda lakini hawajui shughuli yake wengi wanang’ang’ania faida tu…. moja ya masharti ya viwanda watu walitakiwa kuviendeleza lakini kuanzia Ijumaa mimi nitaanza kutenda bila kuwa na maneno.”
“Suala la kiwanda cha Mang’ula tayari mgogoro wake umefika Bungeni na mmiliki wake tayari ameitwa Bunge kuhojiwa, kiwanda cha matairi Arusha tumekiongezea nguvu lakini tunahitaji muwekezaji ataekuwa na nguvu zaidi kwenye uzalishaji.”
“Kiwanda cha General Tyre kina historia kubwa zaidi kilikuwa cha jumuiya ya Afrika Mashariki lakini sasa ni mali yetu, siwezi kumsemea Mh Rais najua ana imani na mimi sana ndio maana nilimuomba asinikumbushe tena siku nyingine.”
“Anayetaka kujua viwanda vingapi vipo mkoa wa Pwani aanzie mkuranga mpaka zegereni kuna zaidi ya viwanda 20 hapo, kiwanda cha Mgololo mufindi kinafanya kazi lakini kuna baadhi ya shughuli nyingine za uzalishaji zinaendelea nje ya nchi.” – Mwijage
VIDEO: RAIS MAGUFULI AFUNGUKA, NI KUHUSU KUTAWALA MIAKA 20
VIDEO: JPM asema wakizuia maziwa yetu kwao na sisi siku hiyohiyo tuzuie yao kwetu, play hapa chini kutazama mwanzo mwisho