Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic amerudi kwenye headlines baada ya maamuzi yake kuandikwa na vyombo vya habari, Zlatan ameripotiwa na mtandao wa dreamteamfc.com kuwa amekataa kulipwa mshahara na Man United.
Zlatan Ibrahimovic atakuwa nje ya uwanja katika kipindi cha miezi 9 baada ya kuumia goti lake la kulia wakati wa mchezo wa marudiano wa Europa League dhidi ya Anderltch ya Ubelgiji, Zlatan anayelipwa mshahara wa pound 250000 kwa wiki alijiunga na Man United kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Baada ya kujulikana kuwa Zlatan atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 9 Man United walikuwa wapo tayari kuendelea kumlipa mshahara kama kawaida katika kipindi chote cha majeruhi lakini Zlatan amekataa, Zlatan anatarajiwa kurudi uwanja kuanzia mwezi Janury 2018.
VIDEO: Adhabu aliyopewa Haji Manara wa Simba na kamati ya nidhamu ya TFF