Michezo

UEFA imemfungia Cristiano Ronaldo

on

Shirikisho la soka Ulaya UEFA baada ya kuanza kuenea kwa tetesi kuwa staa wa Juventus Cristiano Ronaldo kuna uwezekano akakosa mechi zaidi ya moja za michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/19 kwa kuoneshwa kadi nyekundu, UEFA leo imetoa tamko.

UEFA wametangaza kuwa kufuatia kitendo cha Ronaldo kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa kwanza wa Champions League dhidi ya Valencia kwa kumchezea madhambi Jeison Murillo, wengi walianza kuhisi kuwa kuna uwezekano Ronaldo akaongezewa adhabu zaidi kwa kudaiwa kukusudia.

Hivyo kwa maamuzi ya UEFA yaliotangazwa leo ni kuwa Ronaldo atatumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja pekee dhidi ya Young Boys lakini game zilizosalia atakuwa na nafasi ya kucheza, hivyo Ronaldo atakuwa na nafasi ya kucheza game zote mbili za nyumbani na ugenini dhidi ya timu yake ya zamani ya Man United.

JB na Ray “Hata Yanga wao wanajua Simba ana timu bora”

Soma na hizi

Tupia Comments