Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: TOP 10: Nchi 10 duniani zinazotajwa kuwa na kiwango kidogo cha rushwa 2017
Share
Notification Show More
Latest News
Picha: DC Halima Bulembo aungana na wakuu wa Idara, ‘Kutekeleza wajibu wao katika Utumishi’
June 2, 2023
Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi
June 2, 2023
Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.
June 2, 2023
Nyota wa zamani wa Manchester United Lingard kuondoka Nottingham Forest
June 2, 2023
Serikali ya Congo na mahakama ya ICC zakubaliana kuimarisha ushirikiano
June 2, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Duniani > TOP 10: Nchi 10 duniani zinazotajwa kuwa na kiwango kidogo cha rushwa 2017
Duniani

TOP 10: Nchi 10 duniani zinazotajwa kuwa na kiwango kidogo cha rushwa 2017

April 19, 2017
Share
4 Min Read
SHARE

Rushwa ni miongoni mwa vitu vinavorudisha nyuma maendeleo ya nchi nyingi duniani kwani hukwamisha maendeleo na kusababisha kukosekana kwa haki, utawala bora na uvunjifu wa sheria katika nchi nyingi duniani.

Licha ya kuwa rushwa ni tatizo kwa nchi nyingi duniani, lakini kuna nchi zinatajwa kuwa na kiwango kidogo cha rushwa huku sababu kubwa ikitajwa kuwepo kwa utawala bora, uwazi katika kufanya maamuzi na maendeleo ya kiuchumi .

Kwa mujibu wa Corruption Perception Index hizi ndizo nchi 10 zenye kiwango kidogo cha rushwa kwa mwaka 2017.

1: Denmark

Licha ya kuwa miongoni mwa nchi zenye furaha duniani, Denmark inatajwa pia kuwa nchi namba moja yenye kiwango kidogo cha rushwa ambapo kwa mujibu wa Corruption Perception Index nchi hiyo imeweza kupambana na rushwa kwa asilimia 92 kwa mwaka 2017.

2: New Zealand

Ni nchi namba mbili kuwa na kiwango kidogo cha rushwa duniani ambapo sababu kubwa inayofanya nchi hii kuwa na kiwango kidogo cha rushwa ni uwepo wa utawala bora. Serikali ya New Zealand hufanya maamuzi kwa uwazi na hali nzuri ya kiuchumi.

3: Finland

Miongoni mwa sababu inayoifanya Finland kuwa na kiwango kidogo cha rushwa kwa mujibu wa taasisi ya kuchunguza rushwa duniani ni uwepo wa hali ya haki na usawa na hali nzuri ya kiuchumi. Imepata 89%.

4: Sweden

Kwa mujibu wa Katiba ya Sweden, Bunge lina nafasi kubwa ya kufanya maamuzi ukilinganisha na serikali. Hali hii inaifanya serikali ya nchi hiyo kuogopa kufanya makosa ya rushwa kwa sababu ya Bunge kuwa na nguvu kubwa. Aidha, katika nchi hii matumizi mabaya ya madaraka huonekana pia kama rushwa.

5: Norway

Norway ni miongoni mwa nchi zenye kiwango kidogo cha rushwa, na kwa mujibu wa Corruption Perception Index, inapata 86% kwa kuweza kupambana na rushwa kwa mwaka 2017.

6: Switzerland

Switzerland imefanikiwa kupambana na rushwa kwa 86% na kwa mujibu wa taasisis ya kupambana na rushwa, nchi hiyo imefanikiwa kwa sababu Katiba yake inaruhusu wananchi kujihusisha katika majidiliano wakati serikali inafanya maamuzi kupitia njia ya kura za maoni.

7: Singapore

Kwa mujibu wa Corruption Perception Index, Singapore imefanikiwa kwa zaidi ya 84% kupambana na rushwa na inatajwa kuwa nchi ya saba kwa mwaka 2017 kuwa na kiwango kidogo cha rushwa.

8: Uholanzi

Uholanzi ni miongoni mwa nchi zinazotajwa na Corruption Perception Index kwa kuwa na kiwango kidogo cha rushwa ambapo sababu kubwa inayochangia ni uwepo wa program za kuzuia rushwa.

9: Luxembourg 

Inatajwa kuwa moja kati ya nchi ndogo na tajiri zaidi katika nchi za Umoja wa Ulaya ambapo sababu kubwa inayoifanya nchi hiyo kuwa mongoni mwa nchi zenye kiwango kidogo cha rushwa ni hali ya uchumi kuwa nzuri kwa kila raia wa nchi hii.

10: Canada.

Canada ni miongoni mwa nchi zenye kiwango kidogo cha rushwa duniani ambapo moja ya sababu kubwa inayochangia kuwepo kwa kiwango kidogo cha rushwa ni Bunge la nchi hiyo kuwa na nguvu zaidi ya serikali hivyo kupelekea serikali kufanya maamuzi kwa uwazi na utawala bora.

VIDEO: Ilikupita hii ya Wizara ya TAMISEMI kuomba kutengewa zaidi ya Trilioni 6? Bonyeza play kutazama.

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo 

You Might Also Like

Wabunge wafurahishwa na utekelezwaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi EACOP

Profesa Mkenda kufungua maonesho ya Nane ya Tafiti na Ubunifu UDSM

Yanga, UNICEF na Serikali zaungana kutoa elimu Ugonjwa wa Kipindupindu

Harambee ya uchangiaji wa Ujenzi wa shule ya Marian

Dr. Mpango avutiwa na ubunifu wa programu ya IMBEJU

TAGGED: habari daily, Top 10
Admin April 19, 2017
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article VIDEO: Maswali matatu ya Mbunge Professor J Bungeni leo
Next Article VIDEO: Maamuzi ya serikali kuhusu Madaktari 258 waliotakiwa kwenda Kenya
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Picha: DC Halima Bulembo aungana na wakuu wa Idara, ‘Kutekeleza wajibu wao katika Utumishi’
Top Stories June 2, 2023
Upinzani unashinikiza mageuzi mapya ya uchaguzi
Top Stories June 2, 2023
Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.
Top Stories June 2, 2023
Nyota wa zamani wa Manchester United Lingard kuondoka Nottingham Forest
Sports June 2, 2023

You Might also Like

Top Stories

Mlipuko wa ugonjwa wa Marburg umekwisha rasmi Tanzania.

June 2, 2023
Top Stories

Serikali ya Congo na mahakama ya ICC zakubaliana kuimarisha ushirikiano

June 2, 2023
Top Stories

Amnesty yaonya Iran dhidi ya Kunyonga kwa Kesi zinazohusiana na madawa ya kulevya

June 2, 2023
Top Stories

Elon Musk kwa mara nyingine tena ndiye mtu tajiri zaidi duniani

June 2, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?