Rubani wa Air Guilin China amefungiwa maisha kurusha Ndege baada ya kuruhusu Abiria wa kike kuingia chumba cha Marubani na kupiga picha wakati Ndege ikiwa angani ikiwa ni kinyume na kanuni za usalama kwenye Ndege ambapo Rubani huyo amepoteza kibarua baada ya picha hii kusambaa kwenye mitandao.
Picha ilipigwa January 2019 lakini imeibuliwa November baada ya kuonekena na Blogger anaejihusisha na Mambo ya anga ambae alikosoa kitendo hicho, Mrembo huyo alionekana kaweka pozi na vimiminika vikiwa mbele yake na alipoipost kwenye ukurasa wake aliandika “Asante kwa Rubani, nimefurahi sana”
Hii sio mara ya kwanza kwa Rubani kuadhibiwa China, mwaka 2018 Rubani wa Donghai Airlines aliadhibiwa baada ya kumruhusu Mke wake kuingia kwenye chumba cha Marubani wakati Ndege ikiwa angani.
Tangu mashambulizi ya mwaka 2001, Mashirika mbalimbali ya Ndege Duniani yalikoleza Sheria za kukilinda chumba cha Marubani kutokana na hatari ya Magaidi. #MillardAyoUPDATES
VIDEO: MTANZANIA ALIEFUNGWA SOUTH AFRICA ASIMULIA “MWANAMKE ALIPIGA KELELE TUNAPOISHI”
VIDEO: MTANZANIA ALIEBUNI UMEME WAKE “HAUJAKATIKA MIAKA MINNE, NILIISHIA LA SABA”