Serikali ya Kenya imetangaza kununua magari yasio penya mabomu wala risasi ili yasaidie kupambana na magaidi na wezi wa mifugo nchini humo ambapo katika bajeti ya mwaka huu itanunua helikopta ya kisasa kwa ajili ya polisi ilikuongeza wepesi wa polisi kushughulikia mambo ya dharura.
Namkariri akisema ‘magari yasiyo penya risasi na mabomu ni muhimu sana na imejumuishwa kwenye bajeti ya mwaka huu, tuna pania kuimarisha miundo mbinu katika kikosi cha polisi kwa kununua bunduki za kisasa mavazi maalum na vifaa vya mawasiliano, tunajidai kwamba hii ni serikali ya digital lakini vifaa wanavyotumia polisi ni analogue’
Naibu wa Rais William Ruto pia anaunga mkono kuratibiwa kwenye jarida la serikali kwa uwanja wa michezo wa Safaricom Kasarani kua kituo cha polisi kwani idadi kubwa ya washukiwa waliokamatwa kwenye msako wa EastLeigh hawangeenea kwenye kituo chochote cha polisi ingawa yanayoendelea katika uwanja huo si tofauti na yanayofanyika katika kituo chochote cha polisi.