Mkuu wa Idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara ameonesha dhamira yake ya wazi ya kutaka kukata rufaa ya kupinga kufungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka na faini ya Tsh milioni 9 na TFF na leo April 25 ameandika ujumbe katika instagram yake na kuhoji namna ilivyotolewa hukumu hiyo pasipo kuhojiwa.
“Namshukuru Mungu kwa sasa masuala yangu binafsi ya kifamilia nimeyamaliza na naweza sema kitu, kwanza niwape pole nyie kwa haya yaliyonitokea, mimi sio mtu ninayeamini uonevu sio mtu ninayeweza kunyamaza nikiona haki inaporwa, sio mtu mwenye moyo dhaifu wa kuogopa kukosoa pale panapopaswa kurekebishwa”
“Always nitabaki hivyo juzi Ijumaa jioni niliambiwa na ofisi yangu imekuja barua toka TFF, ikiniharifu kuna wito wa kunitaka nifike Karume kusikiliza mashitaka dhidi yangu Jumapili ya jana asubuhi, wakati huo nikiwa Zanzibar kwa masuala yangu ya kifamilia na ofisi ikaiandikia TFF barua ya kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hili hadi Jumanne ya kesho kwa kuwa nitakuwa nipo Dar es Salaam”
“Barua iliwafikia na binafsi nikaongea na Afred lucas msemaji wao na akanijibu ameipokea yeye na imegongwa muhuri na katibu Mkuu wa TFF keshaipata, kumbuka hiyo ni jioni ya Ijumaa, Jumamosi nikampigia Alfred kuulizia kikao hicho cha kamati kimepangwa lini, akanijibu Jumatatu ya leo atanijibu, jana tena mkasikia mliyosikia ni uharaka upi ilionao TFF wa kushindwa kunipa haki ya kusikilizwa?”
“Natural justice nchi hii haitambuliki!! wahaini na wauaji nao pia husikilizwa iweje kwa mtuhumiwa ambae anapigia kelele haki ya mwajiri wake? kuna hoja dhaifu inajengwa kuwa nilipaswa nijibu bnafsi barua ya TFF, hivi ningewezaje kuijibu barua wakati sikuwepo Dar es Salaam na sikuwa nimeiona na vipi klabu yangu isiwe na haki ya kunijibia barua, wakati leo imepokwa haki ya kutokuwa na msemaji?”
“Hivi TFF hawajui kuwa mimi nilikuwa naongea kwa niaba ya ofisi na klabu yangu? nikija sababu za kunifungia nimejiuliza ni kaka yangu huyu Msemwa aliyekuwa anasoma hii hukumu? nimemuona kwa Millard Ayo, anasoma hukumu ilio kinyume na hati ya mashtaka”
“Hati yao ina makosa mengine na hukumu pia nyingine ni aina ya hukumu katili zaidi kwa viwango vya mpira wetu ila nawaambia TFF Haji hajawahi kuwa dhaifu wa moyo, anaweza kuwa dhaifu wa kiwiliwili lakini nina moyo wa Simba, nitapambana kwa kiwango cha juu sana”
“Nitadai haki yangu na mwajiri wangu kwa viwango na nitaziomba kamati zao zipokee rufaa yangu na kukaa kwa uharaka huu walionifanyia na nipewe haki ya kusikilizwa, nisihukumiwe kishabiki wala kwa chuki na nawahakikishia kikao kitakachokaa”
VIDEO: Adhabu aliyopewa Haji Manara wa Simba na kamati ya nidhamu ya TFF