Seba Maganga amezungumza kwenye Clouds TV kupitia kipindi cha Clouds 360 kuhusu hali ya kiafya ya Ruge ikiwa ni baada ya Mkurugenzi mkuu wa Cloud Media Group Joseph Kusaga kusema anaendelea vizuri kiafya na atarejea salama hivi karibuni.
Maganga ameongezea kwa kusema yale mengine ambayo hayajulikani kuhusu Ruge kwa kipindi ambacho amekuwa akihusishwa na mengi kuhusu Afya yake, Seba ameandika……
..>>>“Ni kweli mengi yamezungumzwa lakini ukweli halisi ni huu:… katikati mwezi wa 5 kulelekea mwezi wa 6 hali ya Mkurugenzi haikuwa nzuri na akatuomba kupata muda kidogo ili ashughulikie afya yake na tuliona hili litakuwa dogo tu na tukatoa baraka zote. Lakini ripoti za kitabibu zikasema muda wa kupumzika ni mdogo hivyo akaongezewa muda na katikati ya mwezi wa 6 na wa 7 alirejea na kasi ya kawaida kwenye kazi na wiki mbili tatu tukawa nae na hapo ndiyo tulikuwa tunakaribia kuanza Tigo Fiesta moro. Akatuambia anabidi aelekee kwenye taratibu za kimatibabu na nikiri bado changamoto hizo zipo na madaktari wanakiri Kiongozi wetu ni mpambanaji na bado anahitaji muda wa kupumzika na ni kweli hizo changanoto zilikuwepo”
“Mshirikishe Ruge mutahababkwenye maombi, kumshukuru Rais kutokana na yeye mara baada ya kupata taarifa hizi alinyoosha mkono kwetu na kutuambia changamoto za kiafya ni kubwa na la awali ambalo anataka kulifanya ni kuchangia mfuko wa kiafya na changamoto zisiwe gharama za kimatibabu na kutoa dola elfu 20,000 (karibu million hamsini)”
“Mengi yalizungumzwa na sisi tuliona wakati haukuwa mzuri sana kuzungumza na tuliona tukifanya yoyote na tutaleta maswali mengi ambayo hata yeye hatopenda. Mara nyingi ukipata changamotoA ya kiafya changamoto B inajitokeza na tunashukuru taratibu taratibu hali yake inarudi na kuna hatua kubwa ya kimaendeleo.” – Seba Maganga
Mengine yaibuka kuhusu Ruge, Rais JPM amchangia millioni 50
EXCLUSIVE: Kwa mara ya kwanza Kusaga kazungumzia hali ya Ruge