Club ya Cardiff City ya England bado inaonekana kupambana kutafuta nafasi ya kusalia Ligi Kuu England msimu 2019/2020 kwa kutafuta mshambuliaji sahihi wa kuongeza nguvu katika timu yao.
Baada ya kufuatilia kwa karibu nyendo na uwezo wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta, Cardiff City ilituma ofa ya pound milioni 11.6 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 34 ili kuishawishi Genk iwauzie mchezaji huyo.
Ofa ya Cardiff City kwenda Genk ilikataliwa na sasa imeonekana wamekubali yaishe kwa kumchukua kwa mkopo hadi mwisho wa msimu mshambuliaji wa Everton Oumar Niasse ili awaongezee nguvu, Samatta amekuwa na msimu mzuri na Genk kutokana na kiwango chake kuwa juu akicheza game 31 na kufunga magoli 24 msimu huu katika mashindano yote.
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”