Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amezungumzia suala la Korosho ambapo amesema zinatakiwa zibanguliwe nchini ili kutoa ajira kwa watu wengi wasiokuwa na ajira pamoja na kuiongezea thamani na serikali ipate.
Waziri Hasunga amewaambia waandishi wa habari kuwa serikali imetembelea mikoa inayodhalisha zao la Korosho ambapo wamebaini viwanda vyote vya ndani vilivyopo vipo 23 na uwezo wao ni tani 15, 000 kwa mwaka, huku viwanda vingi vikiwa havifanyi kazi na kugeuzwa kuwa maghara.
“Hatua tuliyoifanya ni kufanya tathmini na hivyo viwanda vifanye kazi mwaka huu, ambapo tayari tushaanza kufanya tathmini ili viweze kurudi katika hali ya awali na viweze kuanza kufanya kazi,”amesema.