Hali ya hewani kuchafuka Bungeni hii Duniani kote iko, ukiyaona leo Bongo sio mageni, kuna wakati utayaona hayo hata kwenye Mijengo ya Mabunge ya wenzetu yaani.
Leo kubwa iliyokaa kwenye kurasa za mbele Magazetini, mitandaoni, ishu ya Wabunge wa upinzani Afrika Kusini kumkatisha Rais Zuma wakati akihutubia Bungeni jana jioni FEBRUARY 12 na kuanzisha mzozo mkubwa wakimtaka Rais huyo aeleze kuhusu tuhuma za Rushwa na Ufisadi zinazomkabili.
“Tunamtaka Rais atujibu majibu mepesi; lini atarudisha pesa zetu“– alihoji Mbunge wa Upinzani, Julius Malema.
Spika wa Bunge Baleka Mbete alimtaka Malema kutoka nje ambapo baada ya kuonekana akibisha kundi la askari walivamia na kumtoa kwa nguvu ndani ya Jengo hilo pamoja na baadhi ya Wabunge, ambapo baadaye Rais Zuma aliendelea na hotuba yake.
Mwezi Novemba 2014 Mbunge Mashabela aliwahi kutamka ndani ya Bunge hilo kuwa Rais Zuma ni mwizi hali ambayo ilichafua pia hali ya hewa kwenye Bunge hilo kwa kiasi kikubwa.
Hii ni video ya tukio la mwaka 2014.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook