Sanamu kubwa ya Yesu Kristo inajengwa huko Kusini mwa Brazil, na itakuwa ndefu zaidi kuliko sanamu maarufu iliyoko katika mji wa Rio de Janeiro nchini humo.
Sanamu ya “Kristo Mwokozi” inajengwa huko katika mji wa Encantado, ambao ni mji mdogo katika jimbo la Kusini kabisa la Brazil la Rio Grande do Sul, na Shirika la nchini humo linaloitwa Friends of Christ Association (AACristo).