Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wanakaa na makundi ya wakulima na wafugaji kujadili kwa pamoja na kutatua migogoro ya ardhi iliyopo.
Samia ametoa agizo hilo wakati akiongea na maelfu ya wakazi wa Chalinze waliojitokeza kumsikiliza wakati akipita kuwasalimia akielekea mkoani Dodoma kwa shughuli za kikazi.
Amesema serikali haiko tayari kuendelea kuona migogoro ya wakulima na wafugaji ikiendelea katika mkoa wa Pwani kwani inarudisha nyuma maendeleo.
Aidha amewataka wafugaji kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule na kuachana na tabia ya kuwaachia mifugo mingi kuichunga jambo ambalo limekua likisababisha migogoro kutokana na kushindwa kuimudu mifugo hiyo na baadae kuingia katika mashamba ya wananchi na kula mazao.
ULIKOSA YA MAKONTENA 100 ‘YAIBIWA’ BANDARINI NI HABARI KUTOKA MAGAZETINI ITAZAME HII VIDEO HAPA