Siku chache baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu Tanzania bara pamoja na visiwani Zanzibar, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC, Jecha Salim Jecha alitangaza kufuta matokeo ya uchaguzi huo huku akitaja kwamba kulikuwa na changamoto kadhaa alizozitaja kuweka kasoro kwenye uchaguzi huo.
Baada ya hapo zilianza ripoti kadhaa kusogelea vyombo vya habari ikafika wakati hata mataifa makubwa kama Marekani walihitaji mzozo na utata wa uchaguzi wa Zanzibar umalizwe.
Aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia CUF leo ameongelea kuhusu kila kitu kilichotokea kuanzia mwanzo wa utata wa matokeo mpaka walipofikia kwa sasa.
Maalim SEIF: ‘Leo tunazungumzia kwa kina suala la Uchaguzi wa Z’bar ikiwemo Salim JECHA kufuta matokeo ya uchaguzi’- #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) January 11, 2016
Maalim SEIF: ‘Kitendo cha Salim JECHA kufuta matokeo kimeleta mgogoro mkubwa Z’bar, uchumi wa Z’bar umeyumba’- #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) January 11, 2016
Maalim SEIF: ‘Uchaguzi ulifanyika kwa amani na bila vurugu, waangalizi wa ndani na nje walitoa taarifa zao pia’- #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) January 11, 2016
Maalim SEIF: ‘Kisheria M’kiti wa Tume ya Uchaguzi hana nafasi kuhoji matokeo yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi’-#MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) January 11, 2016
Maalim SEIF- ‘Matokeo ya Urais yalionesha nimepata kura nyingi zaidi na Dk. SHEIN alikuwa nafasi ya pili’- #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) January 11, 2016
Maalim SEIF: ‘Mkiti Salim JECHA alikiuka Katiba na kuamua kufuta uchaguzi bila kuitisha kikao cha Tume’- #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) January 11, 2016
Maalim SEIF: M’kiti wa Tume alibuni kasoro za uchaguzi yeye mwenyewe na kuzitolea maamuzi yeye mwenyewe’- #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) January 11, 2016
Maalim SEIF: ‘Hoja ya kurudiwa uchaguzi Z’bar haina msingi na haiwezekani kutekelezwa’- #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) January 11, 2016
Maalim SEIF: M’kiti wa ZEC Salim JECHA hafai kuongoza Tume hiyo, anatakiwa akae pembeni, makosa ya uchaguzi aliyafanya yeye- #UPDATES
— millard ayo (@millardayo) January 11, 2016
Maalim SEIF- ‘Tumefanya jumla ya Vikao nane mpaka sasa, nimeshiriki pekeyangu wa CUF na CCM wako watano’- #MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) January 11, 2016
Maalim SEIF: ‘Namuamini Rais MAGUFULI, mazungumzo yetu yalionesha anataka mzozo huu umalizike kila upande umeridhika’-#MillardAyoLIVEUPDATES
— millard ayo (@millardayo) January 11, 2016
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.