Inawezekana tukawa tunafurahia vitu vingi sana katika maisha yetu ikiwemo ukuwaji wa teknolojia na hizi simu zinazorahisisha mambo ila kwa upande mwingine maisha yetu yako hatarini kama hatutokuwa makini, vifo vya watu wanaojipiga picha za selfie vinaendelea kutokea.
Miezi miwili iliyopita headlines za watu kupoteza maisha kwa kupiga selfie ziliingia kwenye headlines kwa mji wa Mumbai India, kutajwa kama ndio mji unaongoza kwa vifo vya watu wanaojipiga selfie duniani.
Ripoti mpya ya tukio la selfie imetokea kwenye mji wa Washington DC Marekani ambako March 3 2016 polisi wamethibitisha kifo cha mwanaume wa mwenye umri wa miaka 43 aliyejiua kwa risasi bila kujua kwamba bastola aliyokua akipiga nayo picha ilikua tayari kufyetuliwa.
Stori ipo ukiplay hii audio hapa chini…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE