Habari za Mastaa

Belle 9 kaelezea kilichotokea mpaka Instagram yake ikaonekana kumtukana Diamond Platnumz

on

March 3 2016 kwenye mitandao ya kijamii moja ya vilivyotambaa sana ilikuwa ni hii ya kumuhusu staa wa bongofleva Belle 9 kuhusu moja ya post iliyokuwa imeandikwa katika account yake ya instagram ikionyesha kumtukana Diamond Platnumz.

millardayo.com ilimpata Belle 9 muda mfupi tu baada ya ishu kutokea na haya ndio yakawa majibu yake >>>Niliamka asubuhi nikakuta calls nyingi, nimepigiwa simu toka saa tisa usiku, nikakuta watu wamenitumia picha na nikachukua hatua ya kuwatumia viongozi wangu hiyo picha

Uongozi wangu uliwapigia uongozi wa Diamond na naamini mambo yameenda sawa, sehemu ambayo wamefeli wale watu ni kumdiss Diamond, baadhi ya wasanii wenzangu wakanishauri na nikampata mtu wa kunirejeshea account yangu

Nadhani ni vizuri kuzilinda hizi account ili kuwe na usalama kwasababu vitu hivi sio vizuri, leo imekuwa tofauti na siku nyingine, yani mtu akinipigia moja kwa moja anaanza kuongelea hiyo ishu sema uzuri ni kwamba wengi hawajaiamini hii sababu sina beef na mtu, mimi sifanyagi hivi vitu ‘ – Belle 9

ULIKOSA KIPISI CHA MOVIE YA MUME KWENDA KAZINI WIFE KULETA MCHEPUKO NYUMBANI? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI…

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments