Serikali ya Tanzania imesema ili kumkomboa mtoto wa kike hasa katika masuala ya kidigatali itajenga vituo 35 pamoja na kuziwezesha shule maalum za Wasichana kupata Miundombinu itakayofanikisha mafunzo ya Tehama kwa watoto wa kike.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa programu ya kumuwezesha mtoto wa kike kuapata mafunzo ya tehama Waziri wa Maendeleo ya Jamii wanawake na makundi maalum, Dkt Dorothy Gwajima amesema vituo hivyo vitawawezesha Wasichana kupata mafunzo ya tehama hata baada ya masomo ya kawaida ili kuendana na kasi ya maendeleo ya kidigitali.
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii kutoka Serikali ya mapinduzi Zanzibar, Riziki Pembe Juma amesema Zanzibar tayari wamesha anza kutekeleza baadhi ya programu zitakazo muinua mtoto wa kike hasa katika masuala ya teknolojia hivyo ujio wa programu ya Umoja wa mataifa inayotekelezwa nchi 11 barani afrika utaongeza thamani katika mafunzo ya teknolojia.