Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Serikali inaridhishwa na mchango wa Sekta ya madini kwenye pato la Taifa na ameitaka Wizara ya Madini kuendelea kushirikiana na wadau ili kuimarisha zaidi sekta hiyo.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jijini DSM katika Mkutano wa kimataifa wa uwekezaji kwenye sekta ya madini na kusema kuwa ili kudhibiti utoroshwaji wa madini Serikali iliamua kuanzisha masomo ya madini na kwamba Serikali inaendelea kutekeleza itifaki zote za madini ili kudhibiti uvunaji haramu wa na kuhakikisha sekta hiyo inazidi kuchangia kwenye pato la Taifa.