Ukizungumzia wanamichezo wanawake matajiri duniani huwezi kuacha kulitaja jina la Maria Sharapova ambaye ni mcheza tennis maarufu. Maria Sharapova ameingia kwenye headlines baada ya kuripotiwa kufungiwa kucheza Tennis kwa muda wa miaka miwili, hiyo ni baada ya vipimo kuthibitisha kuwa anatumia madawa ya kusisimua misuli.
Shirikisho la Tennis la kimataifa duniani (ITF) limemfungia Maria Sharapova baada ya kugundua kuwa amekuwa akitumia dawa hizo za kusisimua misuli aina ya Meldonium kwa muda mrefu.
Shirikisho hilo limetangaza rasmi June 8 2016 kuwa mrembo huyo hatoruhusiwa kucheza tennis kwani amekiuka sheria za michezo, ingawa imetangazwa rasmi kufungiwa kwake, Maria Sharapova anasema yeye amekuwa akitumia dawa hizo kwa matibabu ya moyo tangu mwaka 2006.
ALL GOALS: TAIFA STARS VS MISRI JUNE 4 2016, FULL TIME 0-2
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE