Kumekua na maoni mbalimbali haswa kwa wanawake wajawazito au wanaokua wamejifungua kuwa ni vibaya kula karanga kwa kipindi chote wanachokuwa wananyonyesha au kipindi watoto hao wanapokua wameanza kula wakiwa chini ya mwaka mmoja kwa hofu kuwa itawasababishia allergy watoto hao.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Manitoba Canada watoto 3 kati ya 4 ambao hawakupewa karanga katika umri wao mdogo hupata allergy hiyo ya karanga kwa kipindi ch maisha yao yote jambo ambalo linaweza kuepukika.
Allergy ya karanga kwa watoto inatajwa kuwa na dalili kama mafua makali ambayo baada ya muda huweza kutishia uhai wa anayeumwa na matatizo ya ngozi.
Ulipitwa na hii? “Sina sababu ya kumjibu Godbless Lema kuhusu Lissu” – MUSUKUMA