Mix

Umenifikia mpango wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria mwaka 2016/2017

on

Mei 5 2016 Waziri wa katiba na sheria, Harrison Mwakyembe amewasilisha bungeni mpango wa makadirio ya bajeti kwa mwaka 2016/2017.

Waziri Mwakwembe amesema..>> ‘Wizara yangu itaendelea na uratibu na uimarishaji wa mfumo wa sheria wa nchi na oia juhudi za kuongeza ubora na kuimarisha upatikanaji wa huduma za kisheria na kikatiba sanjari na dhima ya Wizara

Wizara itachukua hatua kuimarisha upatikanaji wa msaada wa kisheria kwa watu wasio na uwezo, kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu na takwimu, aidha Wizara italitumia kwa karibu zaidi jukwaa la haki jinai chini ya Mkurugenzi wa mashtaka.’

Kero zifuatazo zinachelewesha au kukwamisha upatikanaji wa haki sawa kwa wote na kwa wakati

  1. Mazoea ya kila kesi, iwe kubwa au ndogo kuruhusiwa muda mrefu wa upelelezi hata kama mtuhumiwa kakiri kosa.
  2. Upotevu wa mafaili ya kesi pamoja na mahakama kuchukua hatua stahili za kiutendaji na kinidhamu kila upotevu wa mafaili ukitokea.
  3. Ucheleweshaji wa nakala za hukumu na mwenendo wa mashauri.
  4. Ubambikizwaji kesi katika vituo vya Polisi

Ili kufanikisha utekelezaji wa vipaumbele hivi na majukumu yanayoambatana navyo, Wizara yangu inaomba kuidhinishwa kiasi cha Shilingi 35,785,416,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo .

ULIIKOSA KAMA WEWE NI MTUMIJI WA ‘SHEESHA’ KUNA HILI TANGAZO LA SERIKALI, METHADONE JE?

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments