Baada ya timu ya taifa ya Zanzibar Heroes kumaliza nafasi ya pili katika michuano ya Kombe la CECAFA Senior Challenge Cup 2017, ikifungwa na Kenya katika mchezo wa fainali kwa mikwaju ya penati na kuukosa Ubingwa huo.
Timu hiyo iliwasili Zanzibar na kupata mapokezi makubwa licha ya kupoteza mchezo wa fainali kwa penati, ambapo mara nyingi uaminika kuwa inatokea bahati, baada ya mapokezi Rais wa Zanzibar Dr Ally Mohamed Shein ameahidi kutoa viwanja na Tsh milioni 3 kwa msafara wa timu uliyokuwa Kenya.
Rais Shein ametoa zawadi ya viwanja na Tsh milioni 3 kwa kila mchezaji na benchi la ufundi jumla watu 33 waliyokuwa sehemu ya timu ya Zanzibar Heroes nchini Kenya.
Rais Shein amelikubali ombi la kocha wa Zanzibar Heroes Hemed Morocco la kuomba apewe mualiko Rais wa CAF Ahmad Ahmad ili aje aone vipaji vya Zanzibar ili iwe sehemu ya kumshawishi airudishie Zanzibar uanachama wake wa CAF.
“Nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba”-Haji Manara