Ni mwanasiasa wa Zambia anaitwa Frank Bwalya ambae amemiliki headlines kwa kushtakiwa kwa kosa la kumfananisha rais wa nchi hiyo na kiazi ambapo kutokana na mashtaka aliyofunguliwa, akikutwa na hatia anaweza kufungwa jela kwa muda wa miaka mitano.
Siku ya Jumatatu akiwa kwenye radio mwanasiasa huyu wa National Restoration Party (NRP) ambao ni wa upinzani alimtaja rais wa Zambia kama “chumbu mushololwa” na tayari ameshafunguliwa mashataka na kesi itaanza kusikilizwa.
Mwaka 2005 kwenye nchi hiyohiyo ya Zambia mwanaume mmoja alifungwa jela miezi 9 kwa kumuabisha kwenye bar Rais wa kipindi hicho Levy Mwanawasa, mwaka 2002 pia kuna mhariri wa gazeti alikamatwa kwa kumuita Mr Mwanawasa “cabbage” lakini baadae mashtaka yalifutwa.