Bongo Fleva mwaka huu inaweza kumake headlines zaidi kisiasa kama waliotangaza nia wakafanikiwa kushika nafasi hizo wanazoziomba kutoka kwa Watanzania,kuna waliotangaza kugombe Ubunge na wapo waliotangaza kugombea nafasi za Udiwani.
Fid Q alifikiwa na mic ya millardayo.com kutaka kufahamu kama nae ana mpango wowote wa kujiunga na siasa>>’Sijioni kuwa Mwanasiasa ingawa takribani miaka 4 iliyopita na kila siku nakutana na watu wananiambia kuwa nafaa kuwa Mwanasiasa kutokana na uwezo wangu wa kuchanganua mambo ‘
Kwenye sentensi nyingine Fid Q amesema >’Kinachonishinda kwenye siasa kuna siku nilijifunza mapinduzi ni kitu kinachoendelea,tunakaa mtaani tunaimba Malaria mara inakuja Dengue,tunaimba kuhusu mafuriko mara yanakuja mabomu na serikalini kupo hivyo unaingia ndani unakuta kuna mapengo kibao kwa hiyo utaamua mwenyewe kama utakua mkweli au lah na ukitaka kuwa mjuaji sana kuna matatizo yake pia’
Sentensi ya mwisho ya Fid Q ameimaliza kwa kusema >>’Nachokiogopa ni kuwa Mwanasiasa nipate zile hela nyingi halafu nianze kuwa wa uongo hicho ndicho kinachonitisha lakini sioni kama siasa inanishinda naogopa uongo wa siasa’.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos