Bio mwenye umri wa miaka 59, ameanza muhula wake wa pili kama rais wa taifa hilo ambalo limekuwa likikumbwa na changamoto tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya 1991-2002, ikiwemo ugonjwa ebola na uchumi unaodorora.
Kulingana na tume ya uchaguzi, rais Bio alipata ushindi wa asilimia 56 licha ya mpinzani wake mkuu Samura Kamara aliyemaliza wa pili kwa asilimia 41, kupinga matokeo hayo.
Siku ya Jumatatu, Chama cha kamara APC katika taarifa kilishtumu ukosefu wa uwazi na uwajibikaji kutokakwa tume ya uchaguzi, kutokana na kukosekana kwa taarifa kuhusu vituo au wilaya ambazo kura zilikuwa zikitoka.
Kujumlisha kura tayari kulikuwa kumepingwa na chama cha Kamara cha All People’s Congress (APC), ambacho kilishutumu katika taarifa yake Jumatatu madai ya ukosefu wa ushirikishwaji, uwazi na uwajibikaji wa tume ya uchaguzi.
Chama kilidokeza kukosekana kwa taarifa kuhusu vituo au wilaya ambazo kura hizo zilitoka.
Ilikuwa imesema “haitakubali matokeo haya bandia na ya kupikwa”.
Katika taarifa ya baadaye, chama hicho kilidai “kupiga kura kupita kiasi” katika baadhi ya maeneo na kusema “kinaendelea kukataa” “matokeo ya kubuni” na “kuthibitisha ushindi wetu”.
Lakini wafuasi wa Bio walikaribisha matokeo.
“Nina furaha Bio alishinda, tunamtaka kurekebisha uchumi na kuunda nafasi za kazi,” Susan Myers, 34, alisema.
‘Lengo la utawala wangu ujao litakuwa Usalama wa Chakula, kuunganisha faida katika Ukuzaji wa Mtaji wa Watu, kutengeneza ajira kwa vijana wetu, kurekebisha Utumishi wa Umma na kuendeleza teknolojia na miundombinu.
Huu ni ushindi wa pamoja kwa kila mwananchi na lazima tuungane sasa uchaguzi umekwisha kwa lengo la pamoja, ambalo ni maendeleo ya nchi yetu pendwa.
Ninataka kuendelea kuwaonya wananchi wote wa Sierra Leone kuwa watulivu na watii sheria. Hasa, nitoe wito kwa wafuasi wangu kuwa mfano wa kuigwa katika kuwa na amani na utukufu katika ushindi.
Ni lazima tunyooshe mkono wa ushirika kwa kaka na dada zetu wa upande mwingine wa mgawanyiko, kwa kuwa sote tunatafuta kitu kimoja, ambacho ni #amani, #maendeleo na #ufanisi wa Sierra Leone.