Ishu ya ugonjwa wa EBOLA ilichukua uzito kwenye vyombo vya habari kwa mwaka 2014, idadi ya watu waliofariki na kuambukizwa ugonjwa huo Afrika Magharibi ilifanya taarifa hiyo kuwa kubwa duniani.
Tuliwahi kusikia mwaka jana kwamba kuna baadhi ya majimbo Marekani ikiwemo New York kuweka utaratibu wa kuwaweka Karantini watu wote wanaotoka nchi za Afrika Magharibi kwa siku 21 ili kuepusha mazingira ya watu hao kusababisha maambukizi kwa watu wengine.
Taarifa iliyoandikwa zaidi kwenye vyombo vya habari jana na leo kutoka Sierra Leone ni kuhusu Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Samuel Sam-Sumana kujiweka karantini kwa siku 21 kutokana na mmoja wa walinzi wake wa karibu kufariki kwa Ebola.
Amesema katika kipindi hicho chote hatokuwa karibu na mtu yeyote mpaka siku zitakavyoisha.
Kwa nafasi yake ya uongozi kwenye nchi kuchukua uamuzi huo ni ishu ambayo imefanya stori kuwa kubwa sana mitandaoni na kwenye vyombo vya habari.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook